1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Chanjo ya Ebola imeanza kutolewa kusini mwa Kongo

15 Septemba 2025

Shirika la Afya duniani, WHO, limesema utoaji chanjo kwa watu walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola umeanza jana Jumapili kusini mwa jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

WHO inatumai utoaji wa chanjo ya Ebola utazuia kusambaa kwa maambukizi
WHO inatumai utoaji wa chanjo ya Ebola utazuia kusambaa kwa maambukizi. Picha: Luc Gnago/REUTERS

Mlipuko wa ugonjwa huo hatari uliripotiwa mapema mwezi huu kwenye kitongoji cha Bulape na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine 68 wanashukiwa kuwa wameambukizwa. 

WHO imesema dozi za awali zipatazo 400 za chanjo aina ya Ervebo zimetolewa na shehena nyingine ya chanjo itapelekwa siku chache zinazokuja.

Miongoni mwa wanaopatiwa chanjo hizo ni maafisa wa afya walio mstari wa mbele na watu inaoaminika huenda watapata maambukizi kutokana na ukaribu wao na waliokwishaambukizwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW