WHO: China toweni takwimu ongezeko la maradhi ya kupumua
24 Novemba 2023WHO imesema maeneo ya Kaskazini mwa China hasa jiji la Beijing na Liaoning yamerikodi ongezeko la ugonjwa unaofanana na homa ya mafua tangu katikati mwa Oktoba, ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka uliotangulia, huku ikiomba taarifa zaidi kuhusu hali hiyo.
Baraza la afya la taifa laChina limewaambia waandishi habari wiki iliyopita kwamaba ugonjwa huo wa kupumua ulitokana na kuondolewa kwa vizuwizi vya UVIKO-19 na mzunguko wa vimelea vinavyojulikana, ambavyo ni mafua na maambukizi maarugu ya bakteria wanaoathiria watoto, ikiwemo nimonia.
Soma zaidi: Wataalamu: Huenda kukazuka kirusi kipya cha Corona
Baraza hilo la taifa limesema ugonjwa wa mafua utaongezeka zaidi katika msimu huu wa baridi na huenda kukawa na maambukizi mengi katika baadhi ya maeneo katika siku zijazo. Ambapo pia wameonya juu ya hatari ya maambukizi mapya yaUviko-19.
Limesema 'maeneo yote yanapaswa kuimarisha utoaji wa taarifa juu ya magonjwa ya kuambukiza, ili kuhakikisha habari zinaripotiwa kwa usahihi na kwa wakati.
Suala hili limeibuka kufuatia Shirika la Afya Duniani kuiuliza China juu ya data walizorekodi katika 'Mpango wa ufuatiliaji magonjwa yamlipuko' kwenye makundi ya pneumonia isiyojulikana kwa watoto.
Uwazi bado changamoto kwa China
Wakati hilo liendelea, China na WHO bado zinakabiliwa na maswali yahusuyo hali ya uwazi wa kuripoti visa vya mapema zaidi kuhusu Uviko-19 ambayo iliibuka katikati mwa jiji la Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019.
Mwezi huu mamlaka ilianza kutoa ushauri wa masuala ya afya, na kutahadharisha wananchi kusubiri kwa muda katika hospitali zenye watu wengi, lakini bado hazijaweka tahadhari kama ambazo iliweka kipindi cha janga Uviko-19, ikiwemo uvaaji wa barakoa ama kufunga shule.
Soma zaidi: Wataalamu wa WHO watembelea maabara ya Wuhan
Kwa mujibu wa Bruce Thompson, Mkuu wa Shule ya Afya ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Melbourne, '"Data zilifaa kutolewa mapema sana, katika hatua hii, hakuna kitu cha kupendekeza na huenda hii ikawa ni kirusi kipya cha Uviko-19, jambo la msingi ni kuwa tumehakikishiwa kuwa taratibu za ufuatiliaji zinafanyiwa kazi, na hilo ni jambo zuri sana."
Baadhi ya wazazi hukoShanghai, wamesema hawakuwa na wasiwasi juu ya ongezeko la ugonjwa huo, wakati ukionekana kuenea kwa kasi pia walitaraji huenda ungeisha haraka.
Wazazi hao pia wamesema baridi ni hali ambayo hutokea maeneo mengi ulimwenguni, hivyo wanatumaini kuwa watu hawatakuwa na mtazamo tofauti kufuatia janga hilo bali watazingatia utafiti wa kisayansi. Pia wameeleza kua watoto wengi wanaougua sasa hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.