WHO: Idadi ya watu wanaojiua duniani yaongezeka
5 Septemba 2014Matangazo
Ripoti inasema kwamba katika kila sekunde 40 mtu mmoja anajiua.Shirika hilo limelitaja tatizo hilo kama la kiafya ambalo linahitaji kushughulikiwa baada ya kufanya utafiti wake katika nchi 172 duniani.Barani Afrika nchi zilizotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojiua ni Msumbiji,Tanzania,Burundi Sudan Kusini na Uganda.Tanzania iko katika nafasi ya pili barani Afrika ikiwa na asilimia 24.9 ya vifo hivyo vya kukusudia.Je tatizo ni nini? Saumu Mwasimba alimuuliza suali hilo mwanasaikolojia na Mchungaji Robert Mutangwa Ruiza kutoka Iringa Tanzania na alikuwa na haya ya kueleza.
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Josephat Charo