WHO: Mkataba wa majanga wakosa kuafikiwa
11 Mei 2024Lengo lililokusudiwa la kile kinachoitwa 'mkataba wa majanga' ni kuidhinishwa wakati wa Kongamano la Afya Duniani mwaka huu, ambalo ndilo chombo kikuu cha maamuzi cha WHO. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei.
WHO yatafuta mwafaka juu ya rasimu ya makubaliano
Duru ya hivi karibuni zaidi ya mazungumzo ilianza karibu wiki mbili zilizopita huko Geneva nchini Uswisi na yalielezwa kuwa msukumo wa mwisho wa WHO wa kupata mwafaka juu ya rasimu ya makubaliano iliyoko.
Mazungumzo yalianza miaka miwili iliyopita
Lakini baada ya miaka miwili ya mazungumzo, wanachama hao waWHO, walishindwa kuafikiana kuhusu rasimu hiyo kufikia muda wa mwisho wa jana Ijumaa.
Mojawapo ya maswala yenye utata imekuwa ni iwapo na jinsi gani makampuni ya dawa yanapaswa kulazimika kuelezea utaalamu na kuwezesha sehemu ya bidhaa zao kupatikana kwa nchi maskini.