1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Mlipuko wa Ebola, Kongo huenda ulianza muda mrefu

21 Mei 2026

Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko wa Ebola ambao tayari umesababisha vifo vya watu 130 nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huenda ulianza miezi miwili iliyopita.

DR Kongo | Mlipuko wa sasa wa Ebola umewaua watu 130 nchini Kongo.
Mlipuko wa sasa wa Ebola umewaua watu 130 nchini Kongo.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Mtalaamu wa virusi wa shirika WHO Anais Legand amewaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba wamefikia hitimisho hilo baada ya kutathmini ukubwa wa mlipuko na namna ugonjwa huo ulivyosambaa.

Hadi sasa inashukiwa watu wengine zaidi ya 600 wameambukizwa ugonjwa wa Ebola ikiwa karibu wiki moja tangu mlipuko wake ulipothibitishwa kwenye jimbo la Ituri, mashariki mwa Kongo.

WHO imesema inatarajia idadi ya visa vya Ebola itaendelea kupanda na maambukizi yanatarajiwa kwenye nchi jirani na Congo. Hata hivyo, shirika hilo limeondoa uwezekano wa mlipuko wa sasa kuwa janga kwa ulimwengu mzima.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW