1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Mlipuko wa Ebola wazidi kuenea DRC

2 Agosti 2026

Shirika la Afya Duniani, laonya mlipuko wa Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unazidi kuwa mbaya. Changamoto za usalama na ukosefu wa uaminifu zakwamisha juhudi za kudhibiti ugonjwa huo.

DRC Bunia 2026 |
Wataalamu wanaamini idadi halisi ya walioambukizwa Ebola ni kubwa zaidi kuliko visa vilivyothibitishwa.Picha: Anadolu Agency/IMAGO

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema hali inazidi kuwa mbaya ya mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  badala ya kudhibitiwa, huku kukiwa na hatari ya mlipuko huo  kusambaa katika nchi jirani.

Kwa mujibu wa WHO, katika kipindi cha wiki moja iliyopita, visa vipya 567 na vifo 296 vilirekodiwa, idadi kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa ndani ya wiki moja tangu mlipuko huo uanze. Kwa ujumla, visa 3,605 vimethibitishwa maabara, vikiwemo vifo 1,587, huku wagonjwa 651 wakipona.

Aidha shirika hilo linasema juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo zinakwamishwa na ukosefu wa usalama, mapigano ya waasi, idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao na kutokuaminiana kwa baadhi ya jamii.

Wataalamu wanaamini idadi halisi ya walioambukizwa ni kubwa zaidi kuliko visa vilivyothibitishwa, kwani wagonjwa wengi hawafikishwi kwenye vituo vya matibabu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW