MigogoroSudan
WHO: Zaidi ya watu milioni 2 hawana huduma za afya Darfur
26 Machi 2026
Matangazo
Hayo yameelezwa na Shirika la Afya Duniani WHO na afisa mmoja wa shirika la misaada. Shambulio hilo linalotajwa kuendeshwa na jeshi la Sudan, lilisababisha vifo vya watu 70 na kuharibu Hospitali ya Al Daein, ambayo ilikuwa ikiwahudumia watu kote katika jimbo la Darfur Mashariki.
Hayo yakijiri, mapigano yameendelea huku kundi la wanamgambo la RSF likitangaza kuuteka mji wa kimkakati wa Kurmuk, uliopo mpakani mwa Sudan na Ethiopia, huku mamlaka za Chad zikiwazuia wakimbizi wa Sudan kuvuka mpaka wa Al‑Tina, kutokana na sababu za kiusalama.