1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaahidi kujichunguza juu ya jitihada za Ebola

Admin.WagnerD21 Oktoba 2014

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesistiza kuchunga lawama kwamba limekuwa likijikongoja katika kukabiliana na Ebola, ingawa limesisitiza vilevile kuwa lengo kwa sasa lazima liwe kukabiliana na mripuko wa ugonjwa huo.

Zelt zur Isolierung für Fälle von Ebola
Kambi ya kukabiliana na Ebola Guinea BissauPicha: F. Tchuma Camara

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Uswis, Msemaji wa shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa Fadela Chaib, alisema kwa upande wao wanatambua kwamba kuna maeneo mengi yanahitaji kutolewa ufafanuzi katika siku za usoni, na kwamba wanaamini katika kanuni za uwazi na uwajibikaji.

Wakosoaji wamekuwa wakiuliza kwanini WHO litangaze tu, dharura ya afya ya kimataifa mwei Agosti, ikiwa ni takribani miezi minane tangu mripuko huo ulipoanza nchini Guniea. Mgonjwa ambao umedhirisha hatari yake kwa asimia 70 ya visa vyake, umegharimu maisha ya watu zaidi ya 4,500 katika matiafa ya Afrika Magharibi, na kuingia katika rekodi ya juu kabisa ya ugonjwa huo kuwahi kutokea.

Idadi ya visa inapindukia elfu tisa

Kati ya matiafa saba ambayo kumerekodiwa visa zaidi ya 9,200, Liberia Sierra Leone na Guinea kumekuiwa na idadi kubwa zaidi. Wataalamu wanaonya kwamba maambukizi yanaweza kuongezeka na kufikia 10,000 ifikapo Desemba. Msemaji wa WHO mjini Geneva anasema pamoja na takwimu za sasa kutokuwa za uhakika, kutokana na ugumu wa ukusanyaji wake wanatambua kama matiafa hayo matatu yaliathiriwa zaidi yamo katika ripoti yao.

Kituo cha afya Guinea-BissauPicha: F. Tchuma Camara

Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF ambalo limekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya Ebola limesema suala la uhakika wa takwimu limekuwa nje ya udhibiti kwa hivi sasa.

Aidha katika hatua nyingine shirika hilo limesema limefanikiwa kunusurua maisha ya watu 1,000 kutokana na ugonjwa huo hatari kabisa duniani. Katika taarifa yake shirika hilo lilisema limeweza kusaidia zaidi ya wagonjwa 4,500. Miongoni mwa hao 2,700 walibainika kuwa na virus vya Ebola.

Taarifa hiyo ya madaktari wasio na mipaka inasema leo hii katika wakati ambao kwa kiasi kikubwa watu wakiwa na wakati mgumu kwa kutokea vifo na maumviu kumekuwa na simulizi kadhaa za watu walionusurika katika miradi yake iliyopo Guinea, Sierra Leone na Liberia. Kwa hivyo wanayo haki ya kufarahi kwa mafanikio ya kunusuru uhai wa watu 1,000.

Ushahidi wa masikitiko

Baba wa afisa mmoja wa afya anaehudumia MSF, Alexander James anasema amepoteza mke wake, mabinti wawili na kaka yake kutokana na ugonjwa huo hatari. Anasema alikuwa mwenye huzuni sana baada ya mtoto wake ambae anafanya kazi na shirika hilo kwa hivi sasa Kollie James alipolazwa katika kituo cha wagonjwa wa Ebola.

Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda umesema leo kuwa wizara ya afya ya Rwanda inawataka wasafiri wote wanaotembelea nchi hiyo ambao walikuwa Marekani au Uhispania ndani ya siku 22 waripoti hali yao ya kiafya kwa maafisa wa afya. Hii nia hatua ya tahdhari tu ambapo mpaka sasa hakuna kisa kilichoripotiwa nchini humo.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP

Mhariri:

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi