1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUswisi

Mkutano wa mwaka wa WHO waanza Geneva

27 Mei 2024

Mkutano wa mwaka wa Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia afya, WHO umeanza leo Jumatatu mjini Geneva, Uswisi.

Uswisi | Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya, WHO linafanya mkutano wake wa mwaka kuangazia masuala muhimu katika kuimarisha sekta ya afya ulimwenguni Picha: Lian Yi/Xinhua/dpa/picture alliance

Wanachama 194 wa WHO wanapanga kuanzisha miongozo ya vipaumbele vya miaka minne ijayo, ikiwa ni pamoja na mpango wa kuiondoa kabisa Malaria katika baadhi ya mataifa ifikapo 2030, lakini pia hatua ya kukabiliana na ongezeko linaloibua kitisho la usugu wa bakteria, fangasi, virusi, na vimelea.

Hafla ya kutiliana saini mkataba wa WHO kuhusu majanga, iliahirishwa baada ya miaka miwili ya kujadiliwa kwa miaka miwili na kuhitimishwa Ijumaa iliyopita bila ya makubaliano.

Wahusika kwenye majadiliano hayo walishindwa kuafikiana kuhusu masuala nyeti kama vile usambazaji wa dawa, vifaa vya kinga na chanjo wakati kunapotokea majanga huko siku za usoni.

Picha hii ilipigwa 25/03/21 ikionyesha chanjo ya UVIKO-19 ya Oxford/AstraZeneca. Picha: Nick Potts/PA Wire/empics/picture alliance

Kusanyiko hili la sasa linatarajia kuamua juu ya hatua zinazofuata kuelekea kufikia mkataba wa kimataifa.

Soma pia: WHO: Mataifa yakamilishe mkataba wa kudhibiti majanga

MAfunzo yaliyopatikana kutokana na janga la UVIKO-19 yanatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo. Lakini pia kukiwa na matarajio ya kufanyika marekebisho kadhaa ya kimataifa ya WHO ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa kanuni na sheria mpya za kuzuia kuenea kwa magonjwa katika mipaka ya nchi pamoja na wajibu wa kutoa taarifa za milipuko kwa WHO mara moja.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu wa WHO ni "Afya kwa Wote."

Soma pia:WHO yatahadharisha juu ya uhaba wa chanjo ya kipindupindu