1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

WHO yahimiza misaada ya chakula na madawa kwa Tigray

10 Novemba 2022

WHO imesema watu wa Tigray wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula.

Tedros Adhanom Ghebreyesus | Generaldirektor der Weltgesundheitsorganisation WHO
Picha: Salvatore Di Nolfi/dpa/KEYSTONE/picture alliance

Shirika la Afya Duniani WHO limetoa wito hapo jana wa kupelekwa chakula na madawa kwa wingi katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema hadi sasa hakuna msaada ulioruhusiwa.

WHO imesema watu wa Tigray wanahitaji msaada wa haraka baada ya miaka miwili ya vita vya umwagaji damu, wakati kulifikia eneo hilo kukiwa na vizuizi vikali. Je kuna matumaini ya amani Ethiopia?

Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alipongeza mafanikio ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Jumatano iliyopita lakini akasema tayari ni wiki moja sasa na hakuna kinachoendelea katika suala la msaada wa chakula au dawa.

Guterress: Hali inaendelea kuwa mbaya Ethiopia

Mgogoro kati ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray umelitumbukiza eneo la kaskazini mwa Ethiopia katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu.