1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

WHO laelezea wasiwasi juu mashambulizi ya hospitali

18 Julai 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka mashambulizi yanayolenga hospitali na vituo vingine vya kutoa huduma za afya nchini Sudan.

Mzozo nchini Sudan waathiri vituo vya afya
Wagonjwa wakisubiri matibabu katika Hospitali ya Gezira huko Wad Madani nchini Sudan mnamo Septemba 2, 2023. WHO inahofia athari za mashambulizi kwenye vituo vya afya nchini humoPicha: AFP

Mkurugenzi wa WHO kanda ya mashariki mwa Mediterania Hanan Balkhy amesema tangu kuanza kwa vita mnamo mwezi April mwaka jana, shirika hilo limeorodhesha mashambulizi 82 yaliyolenga vituo vya afya ikiwa ni pamoja na mashambulizi 17 katika kipindi cha wiki sita zilizopita

Bi Balkhy ametahadharisha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya kuenea kwa magonjwa kama vile kipindupindu, malaria na homa ya uti wa mgongo.

Vita kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha RSF vimesababisha vifo vya mamia ya watu na kuwaacha maelfu ya wengine bila makaazi.