1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yapaza sauti mzozo wa kiafya Ukingo wa Magharibi

15 Juni 2024

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limetahadharisha kwa mara nyingine juu ya kuendelea kuzorota kwa hali ya kiafya kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi.

Ukingo wa Magharibi | Vikosi vya Israel
Vikosi vya Israel vikipiga doria eneo la Ukingo wa Magharibi.Picha: Nasser Ishtayeh/IMAGO

Hali ya vizuizi, vurugu na mashambulizi yanayoilenga miundombinu ya afya vimefanya iwe vigumu watu kupata huduma kwenye eneo hilo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, WHO, imetoa mwito wa kulindwa raia na huduma za afya kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel.

Taarifa hiyo pia imegusia ongezeko la vurugu na machafuko kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na upande wa mashariki wa mji wa Jerusalem tangu kuzuka kwa vita vya Gaza mnamo Oktoba 7 mwaka jana.

Shirika hilo limetoa takwimu zinazoonesha Wapalestina 521 wameuwawa tangu Oktoba mwaka jana idadi inayojumuisha watoto 126.

Hata hivyo maafisa wa Palestina wanasema idadi ni kubwa zaidi ya watu waliouwawa na vikosi vya Israel au walowezi wa kiyahudi tangu kuzuka kwa vita vya Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW