1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yasema chanjo dhidi ya COVID ziliokoa maisha Ulaya

16 Januari 2024

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa maisha ya watu milioni 1.4 yaliokolewa barani Ulaya baada ya kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 na kutahadharisha kwamba, virusi vya Corona bado vingalipo.

Italien Rom Krankheitswelle
Picha: Cecilia Fabiano/LaPresse/Zuma/picture alliance

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Hans Kluge amewaambia waandishi wa habari kuwa, dozi ya kwanza ya nyongeza dhidi ya UVIKO-19 iliokoa maisha ya takriban watu 700,000.

Kluge ameongeza kuwa ni muhimu kwa watu kuendelea kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya virusi vya Corona, hasa watu walioko hatarini zaidi wakati huu wa msimu wa baridi.

EU yaidhinisha chanjo ya tano dhidi ya Covid-19

Kanda ya Ulaya ya shirika la afya duniani - ambayo inashughulikia nchi 53 zikiwemo zile ya Asia ya Kati - imeorodesha zaidi ya wagonjwa milioni 277.7 wa UVIKO-19 huku zaidi ya watu milioni 2.2 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo unaoshambulia mapafu. 

Takwimu hizo ni za hivi karibuni zilizokusanywa kutoka Disemba 19, mwaka jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW