WHO yasema vituo vyake vimeshambuliwa Gaza
22 Julai 2025
Matangazo
Shirika la afya duniani WHO limesema vituo vyake katika Ukanda wa Gaza vimeshambuliwa na Israel na kusisitiza wito wa nchi za Magharibi kutaka usitishaji mara moja wa vita huku Israel ikiendelea kutanua operesheni zake za kijeshi katika mji wa katikati wa Deir al-Balah.
Mkuu wa shirika la WHO; Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema jeshi la Israel liliingia ndani ya makazi ya maafisa wa shirika hilo, kuwalazimisha wanawake na watoto waondoke kwa miguu na kuwafunga pingu, kuwavua nguo na kuwahoji wafanyakazi wanaume kwa mtutuwa bunduki.
Ghebreyesus pia alilaani shambulio kwenye ghala kuu la WHO huko Deir el-Balah, na aliunga mkono wito wa nchi za Magharibi kutaka vita vikome mara moja, zikisema mateso yamefikia viwango vipya vya kutisha.