WHO: Ruksa kwa washirika wetu kuanza kununua chanjo za mpox
23 Agosti 2024Matangazo
WHO inachukua hatua hii katika juhudi za kutoa chanjo haraka barani Afrika wakati ambapo maambukizi ya virusi vya mpox yanazidi.
Kwa kawaida asasi kama vile Gavi na UNICEF, zinazozisaidia nchi za vipato vya chini kununua dawa zinaruhusiwa tu kununua chanjo baada ya kuidhinishwa, lakini kanuni zimebadilishwa ili kuanzisha mazungumzo juu ya upatikanaji wa chanjo hizo.
Chanjo za aina mbili kutoka Denmark na Japan zimeshapitishwa na wakaguzi. Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC, kimesema baadhi ya chanjo za mpox zilizotolewa kama msaada zinatarajiwa kuwasili barani Afrika wiki ijayo.