1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

WHO yatahadharisha juu ya maafa zaidi nchini Sudan

9 Oktoba 2024

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kanda ya mashariki mwa Mediterania ametahadharisha kuwa vita nchini Sudan vinaweza kugharimu maisha ya watu wengi zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuzuia hali hiyo.

Sudan | RSF | Wakimbizi
Familia zilizohama makaazi yao kufuatia vita kati ya RSF na jeshi la Sudan katika majimbo ya El Gezira na Sennar.Picha: Faiz Abubakr/REUTERS

Tahadhari hiyo imetolewa wakati baa la njaa na maradhi yanaenea huku wafanyikazi wa misaada wakipata changamoto ya kuwasilisha misaada kwa wahitaji.

Balkhy ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Cairo kuwa watoto wenye utapiamlo na akina mama wanakufa kwa kukosa huduma za matibabu huku ugonjwa wa kipindupindu ukisambaa katika sehemu nyingi za Sudan.

Soma pia: Mapigano mapya yautikisa mji mkuu wa Khartoum 

Takriban miezi 18 ya vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vimesababisha mgogoro mkubwa wa wakimbizi wa ndani huku zaidi ya watu milioni 25, sawa na nusu ya idadi jumla ya watu nchini humo wakihitaji msaada wa dharura, chakula na huduma za afya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW