1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yataka misaada zaidi kufikishwa katika Ukanda wa Gaza

12 Agosti 2025

Shirika la Afya Duniani WHO, limeitaka Israel kuiruhusu kupeleka vifaa ya matibabu katika Ukanda wa Gaza, kushughulikia janga la kiafya huko kabla ya Israel haijachukua udhibiti kamili wa ukanda huo.

Schweiz Weltgesundheitsorganisation in Genf
Nembo ya shirika la Afya Duniani WHOPicha: Denis Balibouse/REUTERS

Israel ilisema jeshi lake litaidhibiti Gaza katika mpango ulioidhihnishwa na Baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, hatua iliyokosolewa vikali duniani.

Rik Peeperkorn, mwakilishi wa shirika hilo kwenye maeneo ya Palestina amesema wanataka kupeleka vifaa hivyo Gaza, akilalamika kuwa hata misaada ya kibinaadamu haifikishwi ipasavyo katika ukanda huo licha ya taarifa za awali kusema misaada inafikishwa katika sehemu hiyo inayokumbwa na vita.

Albanese amshutumu Netanyahu kwa hali ya Gaza

"Tunataka kuhakikisha angalau hospitali zinakuwa na vifaa vya kutosha pamoja na dawa. Kwa sasa hatuwezi kufanya hivyo, tunataka pia kujaza upya hifadhi zetu na hatuwezi kwa sasa kufanya hivyo kwa njia inayofaa. Taratibu ni lazima ziwekwe. Tunahitaji kupeleka dawa zote na vifaa vinavyohitajika. Na simaanishi kwa ajili ya afya pekee, lakini pia chakula, masoko lazima yajazwe vyakula, maji, mafuta na kadhalika," alisema Peeperkorn.

Mashirika ya Umoja ya Mataifa yalionya mwezi uliopita kwamba baa la njaa linashuhudiwa Gaza, huku Israel ikizuwia misaada kufikishwa huko. Takriban watoto 12,000 walio chini ya miaka mitano walitambuliwa kuugua utapiamlo mwezi Julai ikiwa ni idadi ya juu kuwahi kurekodiwa Gaza.

  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW