1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yataka nyongeza ya ushuru wa ulevi kupunguza vifo

6 Desemba 2023

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuongezwa ushuru kwa bidhaa za pombe na vinywaji vyenye sukari ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanaokufa kutokana na unywaji pombe na ulaji usiofaa.

WHO inataka ulevi na vyakula vyenye sukari kuongezewa ushuru.
WHO inataka ulevi na vyakula vyenye sukari kuongezewa ushuru.Picha: darksoul72/Pond5/IMAGO

Baada ya kufanya tafiti za viwango vya ushuru, WHO imesema kuwa kiwango cha wastani cha ushuru kimataifa kwa "bidhaa zisizo bora kiafya" kilikuwa cha chini mno, huku ikisisitiza kuwa bidhaa kama vile mvinyo hazitozwi kabisa ushuru katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Soma zaidi: WHO kutanua utolewaji chanjo ya Malaria kwa watoto Afrika

Kulingana na WHO, watu milioni 2.6 hufariki kila mwaka kutokana na kunywa pombe huku watu milioni 8 wakifariki pia kwa mwaka kutokana na ulaji usiofaa.

Shirika hilo limesema kuongeza ushuru kutasaidia kupunguza matumizi ya bidhaa hizo na kutoa motisha kwa makampuni kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa afya ya binaadamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW