1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatangaza timu ya kuchunguza chimbuko la Covid-19

14 Oktoba 2021

Shirika la Afya Duniani WHO, Jumatano lilitangaza timu ya wanasayansi watakaochunguza vimelea vipya na kuzuwia majanga ya baadae, pamoja na kufufua uchunguzi uliokwama kuhusu chimbuko la Covid-19.

 (WHO) Generaldirektor Tedros Adhanom Ghebreyesus
Picha: MOHAMED AZAKIR/REUTERS

Timu hiyo ya wataalamu 26 itakuwa na jukumu la kuandaa mfumo mpya wa kimataifa kwa ajili ya utafiti juu ya vyanzo vya vimelea vya majanga vinavyoinuka na uwezekano wa kuzuka majanga, na majukumu yao yanahusisha pia SARS-CoV-2, ambacho ndiyo kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Mbali na mzozo wa Coivd-19, idadi inayoongezeka ya vimelea vyenye hatari kubwa vimejitokeza na kujitokeza tena katika miaka ya karibuni, ikiwemo MERS, virusi vya mafua ya ndege, Lassa, Marburg ne Ebola.

WHO ilitangaza mapema mwaka huu kwamba itaunda kundi la ushauri wa kisayansi kwa ajili ya vyanzo vya vimelea vipya, kwa kifupi SAGO. Wanachama hao 26 waliotangazwa na WHO walichaguliwa kutoka waombaji 700 na wanatokea katika fani mbalimbali za kisayansi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW