1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

WHO yatarajia makubaliano ya "kihistoria"

22 Mei 2023

Mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaendelea mjini Geneva, huku mkuu wa shirika hilo akitoa wito kufikia makubaliano ya kimataifa juu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Generaldirektor der Weltgesundheitsorganisation (WHO)
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Majadiliano ya mkataba huyo bado yamo katika hatua za mwanzo, yakitarajiwa kukamilika mwaka ujao. Soma pia; WHO kujadili kitisho cha UVIKO-19

Mkutano huu wa kila mwaka ulioandaliwa mjini Geneva kuanzia Mei 21 hadi mei 30 utaamua mustakabali wa haraka na wa muda mrefu wa WHO, kuanzia bajeti ya programu kwa miaka miwili ijayo, maamuzi muhimu kuhusu ufadhili endelevu wa Shirika hilo na mabadiliko yaliyowekwa ili kuboresha michakato na uwajibikaji wa shirika hilo la afya duniani.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo jana Jumapili, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema makubaliano mapya ya kukabiliana na majanga ya kiafya lazima yafikie alichokiita "makubaliano ya kihistoria" yanayoashiria mabadiliko makubwa katika mbinu ya usalama wa afya duniani baada ya mzozo wa Uviko-19.

Soma pia: WHO ina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa ugonjwa wa UVIKO-19 China

Nchi wanachama wameanza mazungumzo kuelekea makubaliano ya kimataifa yenye lengo la kuhakikisha ulimwengu unakuwa na vifaa bora vya kuzuia au kujibu kwa ufanisi zaidi wakati janga litakapotokea. Hata hivyo mchakato huo bado uko katika hatua za awali, lakini lengo ni makubaliano kufikiwa kwa wakati kabla ya mkutano ujao wa Afya Duniani, utakaofanyika Mei 2024.

Taiwani haikujumuishwa

Picha: Walid Berrazeg/Zumapress/picture alliance

Mkutano huu unajiri huku Taiwan ikikosa kujumuishwa katika mkutano huo kufuatia upinzani wa China licha ya madai kwamba msaada na ushirikiano na kisiwa hicho ulikuwa ukiongezeka.

China na Pakistan iliwataka wanachama kukataa kujumuishwa kwa Taiwan, wakati eSwatini na Visiwa vya Marshall zikiunga mkono kujumuishwa kwa kisiwa hicho.

China inadai mamlaka juu ya Taiwan na inasema kisiwa hicho si nchi tofauti bali ni sehemu ya "China moja" inayotawaliwa na Beijing. Msisitizo wa China kwamba Taiwan sio nchi inamaanisha kwamba kisiwa hicho hakijumuishwi na mashirika mengi ya mataifa ya kimataifa.

Taiwan imelaani uamuzi wa shirika la WHO, ikisema "imedharauliwa", na China kuzuia ushiriki wake katika ulimwengu na kwamba Beijing haina haki ya kuzungumza kwa niaba ya kisiwa hicho.

Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan katika taarifa yake imesema serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Taiwanpekee ndiyo inayoweza kuwakilisha watu milioni 23 wa kisiwa hicho katika shirika la WHO na mashirika mengine ya kimataifa na kulinda afya na haki za binadamu za watu wa Taiwan.

Wizara ya mambo ya nje ya China ilisema kabla ya ufunguzi wa mkutano huo kwamba karibu nchi 100 zilionyesha ushirikiano wao kwa kanuni ya China-moja na upinzani wao kwa ushiriki wa Taiwan katika

Mkutano wa Afya Duniani kwa kuandika barua maalum kwa shirika la WHO.

Soma pia;  Taiwan yapuuza vitisho vya China

Taiwan inaruhusiwa kuhudhuria baadhi ya mikutano ya kiufundi ya shirika hilo lakini ilisema kutengwa kwa kisiwa hicho kunazuia juhudi za kupigana Janga kubwa la Uviko 19.

Kisiwa cha Tiawan kinakataa madai ya uhuru wa China na kusema watu wa Taiwan wanaweza kuamua maisha yao ya baadaye.

 

Vyanzo-AFP////https://www.who.int/news/item/19-05-2023-seventy-sixth-world-health-assembly-to-focus-on--saving-lives--driving-health-for-all--as-who-turns-75

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW