1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatoa onyo huku wagonjwa wa surua wakiongezeka duniani

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2024

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua kiliongezeka duniani kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2022 na 2023, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO na lile la Marekani CDC.

Tanzania -chanjo ya surua
Kampeni ya chanjo ya surua nchini TanzaniaPicha: DW

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua kiliongezeka duniani kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2022 na 2023, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO na lile la Marekani CDC.

Takribani watu 110,000 walikufa wengi wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Milipuko mikubwa zaidi ilitokea katika nchi ambazo watoto walikuwa na lishe bora na wangeweza kustahimili ugonjwa huo na ambako kulikuwa na huduma bora za afya.

Mamlaka hizo za afya duniani zimesema surua, moja ya magonjwa ya kuambukiza duniani unaweza kuzuilika kupitia dozi mbili za chanjo.

Duniani kote asilimia 83 ya watoto hupatiwa chanzo ya kwanza lakini ni asilimia 74 wanaopokea chanjo ya pili. Jumla ya nchi 57 ziliripoti milipuko ya surua mwaka 2023, karibu nusu zikiwa za Afrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW