1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatoa tahadhari katika kukabiliana na Ebola

18 Mei 2026

Shirika la Afya duniani WHO limetoa tahadhari ya kimataifa katika kukabiliana na mlipuko mpya wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya mtu wa kwanza kuambukizwa Goma.

Querschnitt I Ebola Virus
Bundibugyo ni aina mpya ya virusi vya Ebola vinavyodaiwa kuwa hatari na ambavyo vinasambaa kwa kasi katika mikoa ya kivu kaskazini na Ituri.Picha: IMAGE POINT FR/NIH/NIAID/BSIP/picture alliance

Kulingana na takwimu za hivi punde zilizotolewa na Kituo cha kudhibiti na kupambana na magonjwa ya milipuko barani Afrika, (Africa-CDC), vifo 88 vinavyowezekana kuwa vimetokana na virusi hivyo vimeorodheshwa na takribani watu 336 wanashukiwa kuwa wameambukizwa. Kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 59 raia wa Kongo kiliripotiwa pia katika nchi jirani ya Uganda.

Wakiwa na hofu kufuatia tangazo hilo kuhusu mtu wa kwanza kuwa ameambukizwa Ebola mjini Goma, baadhi ya wananchi wanaelezea hisia zao.

"Tunasumbuliwa sana , hatujuwe tufanye je, uhaba wa pesa utudandamize, vita na hivi sasa ni Ebola hatujuwe chakufanya . tunawaomba viongozi wetu watusaidiye. Ona hata mpaka kati ya Rwanda na DRC umefungwa shida kubwa kwetu sababu ya Ebola ". Tunaomba viongozi wafunguwe uwanja wa ndege ili tupate misaada yakukabiliana na Ebola.

Bundibugyo aina mpya ya virusi vya Ebola

Katika tangazo lao ,Uongozi wa wapiganaji wa AFC /M23 wanaodhiiti mji wa Goma umesema kuwa mgonjwa aliye gunduliwa kuwa na Ebola ni mkazi wa jimbo jirani la Ituri ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka . Desiré NGABO KISUBA  ni meya wa jiji la Goma.

"Tumewaomba watu wate wanaokuwa na migahawa , hao wenyeji wa makanisa kuheshimu kanuni za Afya kwakuweka maji mbele ya mlango ili kila yule anayeingia aelewe kinachoendelea.Ikiwa kutaripotiwa na kifo tafadhi ,msiguse maiti."

Bundibugyo ni aina mpya ya virusi vya Ebola  vinavyodaiwa kuwa hatari na ambavyo vinasambaa sasa kwa kasi katika mikoa ya kivu kaskazini na Ituri.

Kongo imekumbwa na mlipuko mkubwa wa Ebola siku zilizopita. Mlipuko mbaya ulisababisha karibu vifo 2,300 na karibu watu 3,500 waliambukizwa kati ya mwaka 2018 na 2020.

Vyanzo vya ndani vimesema, siku ya Jumapili, mamia ya watu wakiwemo wafanyabiashara wadogowadogo wilikwama kwenye mpaka kati ya Rwanda na Congo upande wa Goma na Rubavu baada ya nchi hiyo jirani kufunga mpaka wake ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Hata hivyo, Mamlaka katika mji wa Goma, zimeeleza kuwa mikakati thabiti tayari imewekwakama kuwekwa ndoo za maji katika sehemu zote za umma ili kukabiliana na maambukizi hayo hatari.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW