1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WIESBADEN: Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wakutana

2 Machi 2007

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walikutana jana mjini Wiesbaden hapa Ujerumani kuzungumzia eneo la Balkan, huku kukiwa na matumaini ya kufikiwa makubaliano kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo na kwamba Bosnia itaendelea kuwa na utulivu.

Akizungumza kuhsu mataifa ya Balkan, mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, alisema,

´Ningependa kusema kwamba Bosnia, Serbia na Kosovo ni sehemu ya bara letu, kwa hiyo utulivu wao ni muhimu kwetu. Na tunajukumu la kuzipa nafasi ziijongelee Umoja wa Ulaya katika siku za usoni na hatimaye kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya.´

Katika mkutano huo wa siku mbili uliofanyika magharibi mwa Ujerumani, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walipendekeza kupunguza idadi ya wanajeshi nchini Bosnia kufikia 2,500 mwaka huu kutoka wanajeshi 6,500 walio nchini humo kwa wakati huu. Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia kuimarika kwa usalama nchini Bosnia.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, amesema wanapanga kuwaondoa wanajeshi 3,500 kwanza na watasubiri matokeo kabla kuendelea kuwapunguza zaidi wanajeshi walio nchini Bosnia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW