Wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda
7 Aprili 2005
Matangazo
Wiki ya makumbusho ya Wanyarwanda waliouwawa katika mapigano ya kimbari imeanza hivi leo katika wilaya ya Murambi, Kaskazini mwa Rwanda. Maadhimisho hayo yanawakumbuka Wanyarwanda zaidi ya laki 8 waliouwawa katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Maadhimisho hayo ni ya 11 tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda. Hali kadhalika shughuli za maziko ya masalia ya miili ya watu waliouwawa katika mauaji hayo zimefanyika katika mikoa mbalimbali nchini humo.