1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wimbi la joto kali laitikisa Ulaya Magharibi

26 Mei 2026

Wimbi la joto kali limezikumba nchi kadhaa za Ulaya Magharibi na kusababisha serikali kutoa tahadhari za hatari kwa wananchi.

Frankfurt am Main 2025 | Umuhimu wa kunywa maji
Watalaamu wameshauri watu kunywa maji kwa wingi wakati wa joto kali UlayaPicha: Florian Wiegand/Getty Images

Watu kadhaa wameripotiwa kuzama maji nchini Uingereza na Ufaransa walipokuwa wakijaribu kujipooza kutokana na joto kali.

Uingereza imerekodi kile kinachoitwa "usiku wa kitropiki", hali ambayo joto halishuki chini ya nyuzi 20 katika kipimo cha Celcius. Idara ya hali ya hewa nchini humo imeonya kuwa viwango vya joto vinaweza kupanda hadi nyuzi 35.

Ufaransa pia imeshuhudia joto kali ambapo jana Jumatatu ilirekodi nyuzi 36 na usiku kucha joto likabaki juu ya nyuzi 20.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Maud Bregeon amesema kulikuwa na taarifa za vifo saba vinavyohusishwa na joto kali—watu watano waliozama na vifo viwili vilivyotokea wakati wa mashindano ya michezo. Serikali nchini humo imetangaza hatua za dharura, ikiwemo kuongeza vituo vya kupoozea joto na kuimarisha huduma za afya katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Wataalamu wa hali ya hewa wanasema ongezeko la joto duniani linaongeza uwezekano wa kutokea kwa matukio makali ya hali ya hewa katika nyakati zisizotarajiwa na katika maeneo ambayo hapo awali hayakuwa yakipata joto kali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW