1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WINDHOEK : Rais mpya wa Namibia aapishwa

22 Machi 2005

Rais mpya wa Namibia Hifikepunye Pohamba ameapishwa rasmi na ameanza kuuda serikali yake.

Pohamba ameapishwa mbele ya watu 20,000 katika mji mkuu wa Windhoek.Pohamba amejipatia ushindi wa zaidi ya asilimia 70 ya kura katika uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi wa Novemba mwaka jana.Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 amesema anataka kulipa kipau mbele suala la kugawa ardhi upya kutoka kwa wakulima wa kizungu na kuwapa wazalendo.

Pohamba anakuwa kiongozi wa pili wa taifa hilo lenye utajiri wa madini ya almasi tokea lilipojipatia uhuru wake kutoka Afrika Kusini hapo mwaka 1990.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW