WINDHOEK:Mataifa ya magharibi yakashifu uongozi wa Zimbabwe
21 Machi 2007Mataifa ya magharibi yanasisitiza kuunga mkono vyama vya upinzani nchini Zimbabwe huku Rais Mugabe akitisha kuwafurusha mabalozi wa mataifa ya kigeni wanaoendelea kumkashifu.Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek-Zeul anatoa wito kwa nchi jirani kushtumu uongozi wa Rais Mugabe unaokiuka haki za binadamu.
Wakati huohuo Rais wa Zambia Levy Mwanawasa anatoa wito kwa mataifa wanachamama wa Jumuiya ya Maendeleo ya mataifa ya Afrika Kusini, SADC kuingilia kati suala hilo na kujadilia matatizo yanayokumba Zimbabwe.
Hata hivyo kiongozi huyo aliyekuwa ziarani kwa siku tano nchini Namibia anaongeza kuwa mataifa yasiyo wanachama wa jumuiya hiyo ya SADC yasihusike.
Zimbabwe inalaumu mataifa ya magharibi kwa kuingilia nchi yake kufuatia shutma kutoka Umoja wa Ulaya,Uingereza na Marekani baada ya kushambulia wanasiasa wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ,MDC.