1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Wine akiri yuko mafichoni, akiukimbia utawala wa Museveni

23 Januari 2026

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amedai kwamba amekimbilia mafichoni baada ya kuvamiwa na wanajeshi nyumbani kwake.

Uganda Kampala 2026 | Kiongozi wa upinzani Bobi Wine katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa rais
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea urais wa (NUP) Robert Kyagulanyi Ssentamu, Bobi Wine akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari nyumbani kwake Kampala mnamo Januari 15, 2026, wakati wa uchaguzi mkuu wa Uganda wa 2026.Picha: Rian Cope/AFP/Getty Images

Wine ameiambia DW kwamba wanajeshi waliagizwa na Mkuu wao Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais Yoweri Museveni aliyepambana naye kwenye uchaguzi wa wiki iliyopita na ambaye anaamini alimshinda.

Bobi Wine amesema anahofia usalama wake huku akiishutumu familia ya rais kwa kuchukua hatua kinyume cha sheria, akiongeza kuwa wanafanya wanachokitaka na tayari amearifiwa kwamba wanataka kumdhuru.

Mwanasiasa huyo amesema, hakuna na namna nyingine zaidi ya kujificha kwa kuwa hakuna taasisi yoyote ambayo ingeweza kumlinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW