1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

WItkoff akutana na Netanyahu kuhusu usitishaji vita Gaza

20 Oktoba 2025

Mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff pamoja na mkwe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner, wamekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Netanjahu, Witkoff na Kushner wakutana Israel
Witkoff na Kushner wamekutana na Benjamin Netanyahu nchini Israel baada ya mkataba wa usitishaji vita kati ya israel na wanamgambo wa Hamas kukumbwa na kitisho cha kusambaratikaPicha: Chen Junqing/Xinhua/IMAGO

Mkutano huo nchini Israel unalenga kujaribu kunusuru mkataba wa usitishaji vita Gaza.

Hii ni baada ya mkataba huo tete kukumbwa na mtihani mkubwa pale Israel iliposema wanamgambo wa Hamas wamewaua wanajeshi wake wawili.

Jeshi la Israel limesema limeanza tena kuhakikisha makubaliano ya usitishaji vita yanatekelezwa na kwamba misaada itaanza kuruhusiwa kuingia Gaza.

Ni zaidi ya wiki moja sasa tangu mkataba wa usitishaji vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ulipoanza kutekelezwa.

Tangu mkataba huo ulipoanza, wanamgabo wa Hamas wameingia mitaani na kumetokea makabiliano na magenge mengine yenye silaha.

Awamu inayofuata ya mkataba huo inatarajiwa kuangazia kuipokonya Hamas silaha na kuondoka zaidi kwa vikosi vya Israel katika maeneo mengine ya Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW