Witkoff kufanya mazungumzo Berlin kuhusu Ukraine
13 Desemba 2025
Matangazo
Afisa mkuu huko Washington amelithibitisha shirika la habari la dpa kwamba Witkoff atasafiri kuelekea Berlin wikendi hii kwa mkutano huo lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu mfumo wa mazungumzo hayo.
Wakati huohuo, kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, anatarajiwa kukutana na Zelensky na viongozi kadhaa wa Ulaya ikiwa ni pamoja na wakuu wa Umoja wa Ulaya na jumuiya kujihami ya NATO siku ya Jumatatu.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer pia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika katika majengo ya ofisi ya Kansela huyo.