1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Witkoff: Mazungumzo ya amani Ukraine yanakaribia mwisho

22 Januari 2026

Witkoff amesema mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Ukraine yamepiga hatua kubwa, na kwamba sasa limebaki suala moja tu muhimu ambalo pande husika zinahitaji kulikamilisha kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya mwisho.

Uswisi Davos 2026 | WEF | Steve Witkoff na Jared Kushner
Mjumbe Maalum wa Marekani Steve WitkoffPicha: Chip Somodevilla/Getty Images

Akizungumza katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Witkoff ameeleza kuwa Ukraine na Urusi zimeonyesha utayari wa kushughulikia suala hilo la mwisho, na akasisitiza kuwa matarajio ya kupatikana kwa suluhu ya kudumu bado yako juu.

"Nadhani tumepiga hatua kubwa. Nafikiri mwanzoni mwa mchakato huu kulikuwa na mkanganyiko kidogo. Nilikuwa nikienda Moscow mara kwa mara, lakini naamini ilikuwa ni muhimu kwenda huko kwa sababu sasa tumefika mwisho wa mchakato, na nina matumaini makubwa."

Mjumbe huyo maalum wa Marekani amesema Washington imekuwa ikifanya mazungumzo ya kina na Urusi, pamoja na Kyiv na viongozi wa Ulaya, kupitia rasimu mbalimbali za mpango wa kumaliza vita vinavyoendelea.

Hata hivyo, licha ya juhudi hizo na ahadi za mara kwa mara kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump kwamba makubaliano yatapatikana, bado hakuna mkataba wa mwisho uliotiwa saini.

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano wa Davos siku moja kabla, Trump aliwataka viongozi wa Urusi na Ukraine kuonyesha busara na kufikia makubaliano, akisema kuwa itakuwa "ujinga" kwao kushindwa kutumia fursa iliyopo ya kumaliza vita hivyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW