Wito kuzingatia upya malipo ya ruzuku kwa viwanda
20 Januari 2008Matangazo
BERLIN: Kamishna wa Viwanda katika Umoja wa Ulaya, Guenter Verheugen amependekeza kuzingatia upya sera ya kutumia pesa za umma kuvilipa ruzuku viwanda.Suala hilo limezuka baada ya kampuni ya simu za mkononi-Nokia-kutangaza kuwa kiwanda chake mjini Bochum katika jimbo la Ujerumani la North Rhine Westphalia kitafungwa na kazi zake zitahamishwa nchini Rumania kwa sababu zinazohusika na gharama za mishahara.
Tangazo hilo limesababisha hasira kubwa nchini Ujerumani kwa sababu Nokia imepokea msaada wa kama Euro milioni 80 kutoka serikali ya jimbo hilo na serikali kuu ya Berlin.Kiasi ya watu 2,300 watapoteza nafasi zao za kazi na wengine 2,000 katika makampuni yanayohusika kikazi na Nokia.