WITO WA WHO KUISAIDIA IRAN:
1 Januari 2004Matangazo
TEHRAN: Katika kipindi cha siku mbili za nyuma si chini ya watu 5 wamekutikana wakiwa hai chini ya nyumba zilizoteketezwa na mtetemeko wa ardhi katika mji wa Bam.Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.Kwa wakati huo huo maafisa wamesema idadi ya vifo katika maafa makubwa kabisa ya miongo hii ya karibuni huenda ikafikia 40,000.Matumainio ya kukuta watu walio hai yakififia,makundi mengi ya wasaidizi yamesita sasa kusaka watu.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limeeleza wasi wasi wake mkuu kuhusu hali zinazowakabili watu walionusurika na limeomba msaada wa Dola milioni 3.5. Kwa mujibu wa WHO pesa hizo zitaisaidia serikali ya Iran kuongeza bidhaa zinazohitajiwa,kutengeneza vifa vya hospitali vilivyoharibika na kutoa huduma za tiba katika mji wa Bam.Sasa katika mji huo ulioteketezwa kwa mtetemeko,kuna kiasi ya watu 40,000 kutoka umma wa zamani wa 103,000.