1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Wito watolewa Haiti na Jamhuri ya Dominica kumaliza mvutano

19 Septemba 2023

Afisa wa Umoja wa Mataifa, ametoa mwito kwa serikali ya Haiti na Jamhuri ya Dominica kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kutafuta mwafaka juu ya mvutano uliosababisha kufungwa mipaka baina ya mataifa hayo jirani.

Mto Massacre unaokatisha Haiti na Jamhuri ya Dominica
Mipaka yote kati ya Haiti na Jamhuri ya Dominica imefungwa tangu Ijumaa ya Septemba 15, 2023.Picha: Ricardo Hernandez/AP Photo/picture alliance

Afisa huyo, William O´Neill, anayeshughulikia masuala ya haki za bindamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti, amesema kufungwa mipaka ya nchi hizo kutaathiri ajira na biashara kwa raia wa pande mbili.

Pia ametahadharisha juu ya taathira kubwa  katika upatikanaji wa bidhaa muhimu upande wa Haiti.

Jamhuri ya Dominica ilitangaza siku ya Ijumaa kuzifunga njia zote za mipaka na Haiti kupinga ujenzi wa mfereji utakaochepusha maji ya mto Massacre unaokatisha kwenye nchi hizo mbili.

Serikali ya nchi hiyo inasema ujenzi huo utaharibu mazingira na kutishia ustawi wa wakulima wa Jamhuri ya Dominica. Haiti kwa upande wake inasema inahitaji maji hayo ili kupunguza makali ya ukame kwenye wilaya yake ya Maribaroux.

O´Neill amezihimiza pande hizo mbili kutafuta suluhu kwa njia ya amani au ziombe usuluhishi wa kimataifa iwapo itahitajika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW