Wito watolewa kuwasaidia watoto wanaotumika vitani
5 Desemba 2024Beah ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watoto hao hawapaswi kuachiwa kutumika vitani.
Wakati wa ziara yake wiki hii katika mji wa mashariki wa Port Sudan, Beah ambaye pia ni balozi wa nia njema wa Shirika la Umoja wa Mataifa Kuwahudumia Watoto, UNICEF, ambaye pia alisajiliwa kwa nguvu katika kundi la wanamgambo nchini Sierra Leone akiwa na umri wa miaka 13, alikutana na watoto na familia zilizopoteza makazi yao.
Soma pia: Wanajeshi 250 wa Sudan Kusini waondoka Kongo
Baada ya ziara hiyo, Beah alisema imekuwa vigumu kuona kile alichokipitia miaka mingi iliyopita bado kinatokea kwa watu.
Beah anasema vijana wengi aliokutana nao walionekana kuwa wakakamavu huku wakiwa na nia ya kuusimulia ulimwengu hadithi zao.
Beah anasema ujumbe ambao wote walirudia tena na tena ulikuwa, ulimwengu unaweza kusaidia kukomesha vita.