1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Afya Gaza yasema idadi ya vifo yafikia watu 44,235

25 Novemba 2024

Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema watu 44,235 wameuawa katika ukanda wa Gaza katika zaidi ya miezi 13 ya vita kati ya Israel na Hamas.

Hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza
Hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Hatem Khaled/REUTERS

Idadi hiyo inajumuisha vifo vya watu 24 vilivyotokea saa 24 zilizopita.

Kulingana na takwimu za wizara hiyo ya afya, watu wengine 104,638 wamejeruhiwa huko Gaza tangu vita vilipoanza baada ya wapiganaji wa Hamas kuishambulia Israel mnamo Oktoba 7, mwaka uliopita.

Wakati hayo yanaarifiwa, mamlaka ya Palestina imesema Wapalestina wawili, akiwa mvulana wa umri wa miaka 13, wameuawa katika uvamizi wa Israel katika kijiji cha Yabad, eneo la ukingo wa Magharibi unalokabiliwa kimabavu na Israel.

Shirika rasmi la habari la Palestina Wafa limeripoti kuwa, wanajeshi wa Israel walivamia kijiji hicho jana Jumapili na kusababisha mapigano ambapo baadaye wanajeshi hao waliwapiga risasi Wapalestina wawili.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW