1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wizara ya afya Gaza yasema watu 39,145 wameuawa katika vita

Josephat Charo
24 Julai 2024

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema hivi leo kwamba watuw apatao 39,145 wameuliwa katika kipindi cha zaidi ya miezi tisa ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa kundi la Hamas.

Vita vya Gaza
Mlipuko uliotokana na shambulio la anga la Israel huko GazaPicha: Omar Naaman/REUTERS

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema hivi leo kwamba watuw apatao 39,145 wameuliwa katika kipindi cha zaidi ya miezi tisa ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa kundi la Hamas.

Soma: Israel yaendelea kuvurumisha mashambulizi ya ardhini Gaza

Kwa mujibu wa takwimu za wizara hiyo, idadi hiyo inajumuisha vifo 55 vilivyotokea katika saa 24 zilizopita. Wizara hiyo imewaoredhesha watu 90,257 ambao wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu vita vilipoanza wakati wanamgambo wa Hamas walipoishambulia Israel mnamo Oktoba 7 mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW