1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Palestina: Israel yasababisha vifo Ukingo wa Magharibi

21 Novemba 2025

Wizara ya afya ya Palestina imesema kuwa vikosi vya Israel vimewaua kwa kuwapiga risasi vijana wawili katika mji wa Kufr Aqab, katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Mzozo wa Mashariki ya Kati
Wizara ya afya ya Palestina yasema watu wawili wameuwawa katika machafuko ya Ukingo wa Magharibi Picha: Ben Stansall/AFP/Getty Images

Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema vijana waliouwawa ni Amr Khaled Ahmed Al-Marbou aliye na umri wa miaka 18, na Sami Ibrahim Sami Mashayekh aliye na umri wa miaka 16.

Jeshi la Israel pamoja na polisi wanaodhibiti eneo hilo hadi sasa hawajasema lolote kuhusu tukio hilo na wala kujibu ombi la shirika la habari la AFP, kuwataka watoe maoni yao juu ya mauaji hayo. Kulingana na shirika la hilali nyekundu lililowapeleka vijana hao hospitalini, wote wawili waliovalia vesti ya kujikinga na risasi walijeruhiwa vibaya vifuani. 

Adi al-Shurfa, ambae ni rafiki ya Al Marbou aliyeshuhudia kisa hicho amesema wote wawili walikuwa nje wakati wa machafuko kati ya jeshi la Israel na raia wa Palestina, kabla ya kupigwa risasi. Amesisitiza rafiki yake hakuwa anarusha mawe wala kushiriki katika machafuko hayo.

    

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW