1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Uingereza yasema Urusi imeanza mashambulizi mapya Vuhledar

31 Januari 2023

Uingereza imesema Urusi imeanza mashambulizi mapya makubwa kwenye ngome ya Vuhledar inayoishikilia nchini Ukraine ambayo huenda ikawa na faida ya ndani lakini hakuna uwezekano wa kusababisha mafanikio ya kiutendaji.

Ukraine Krieg | Bachmut
Picha: Marek M. Berezowski/AA/picture alliance

Ukraine imesema imezuia mashambulizi dhidi ya Vuhledar na Blahodatne, kijiji kilichoko kaskazini mwa Bakhmut. Msimamiziwa maeneo yanayodhibitiwa na Urusi ya jimbo la Mashariki la Donetsk, Denis Pushilin, amesema vikosi vya Urusi vimeshikilia udhibiti katika eneo la Vuhledar. Katika taarifa za kijasusi za hivi karibuni, wizara hiyo ya Uingereza imesema kuwa Urusi imekuwa ikishambulia mji huo wa uchimbaji wa mkaa wa mawe kwa nguvu kubwa kiasi cha maelfu ya wanajeshi. Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kuna uwezekano wa uhakika kwamba Urusi itaendelea kupata ufanisi wa kimaeneo katika sekta hiyo. Hata hivyo, hakuna uwezekano kwamba Urusi ina wanajeshi wakutosha ambao hawajajitolea katika eneo hilo ili kufikia mafanikio makubwa kiutendaji.

Mashambulizi ya uchokozi yafanywa katika eneo la Bakhmut

Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema Urusi imefanya mashambulizi ya angani na mashambulizi matatu ya makombora katika muda wa saa 24 zilizopita, moja katika eneo la Kharkin Kaskazini Mashariki mwa Ukraine. Pia mashambulizi ya uchokozi yamefanywa katika maeneo ya Bakhmut, Avdiivka na kwengineko Mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo, shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ripoti hiyo ya eneo la mapambano. Haya yanajiri wakati ambapo Ukraine imesema inatarajia kupokea takriban vifaru 140 baada ya washirika wake wa Magharibi kukubalina mapema mwezi huu kupeleka silaha nzito nchini Ukraine kufuatia wiki kadhaa za mashauriano.

Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Susan Walsh/AP/picture alliance

Wakati huo huo, alipoulizwa jana na mwanahabari mjini Washington ikiwa Marekani itatuma vifaru aina ya F-16 nchini Ukraine, rais wa Marekani Joe Biden alijibu tu kwa kusema hapana. Matamshi yake yanakuja baada ya kueleweka kufikisa sasa kwamba serikali ya Marekani haijatupilia mbali uwezekano wa kutuma mfumo wowote wa silaha na kwamba ilikuwa inakadiria msaada wake kwa Ukraine kulingana na mahitaji yake.

Ufaransa yakubali kutuma ndege Ukraine kwa masharti

Siku ya Jumatatu, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, alisema kuwa Ufaransa haizuii kutuma ndege za kivita nchini Ukraine, lakini imeweka masharti mengi kabla ya hatua hiyo muhimu kuchukuliwa. Miongoni mwa masharti hayo ni kwamba kutolewa kwa silaha hizo hakutasababisha kuongezeka kwa mvutano ama kutumiwa nchini Urusi na kwamba hazitadhoofisha uwezo wa jeshi la Ufaransa. Macron pia amesema kwamba Ukraine itabidi kutuma maombi rasmi ya ndege hizo.  Ufaransa imeitumia Ukraine mifumo ya ulinzi ya anga, vifaa vya kurusha roketi, mizinga na vifaa vingine vya kijeshi na imeahidi kutuma vifaa vya ufuatiliaji wa kivita na magari ya vita, lakini haijatuma mizinga ya vita au silaha nzito zaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW