1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Ulaya haijajiandaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi"

17 Februari 2026

Umoja wa Ulaya haujajiandaa ipasavyo kukabiliana na matukio yanayoongezeka na yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

WMO yatahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi
Ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi huko UhispaniaPicha: Emilio Morenatti/AP/dpa/picture alliance

Ulaya inapaswa kuongeza uwekezaji wake haraka ili kuwalinda watu na miundombinu kutokana na mafuriko, moto wa nyika na  joto kali. Hayo yameelezwa leo na washauri wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) waliotahadharisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yameifanya  Ulaya kuwa bara lenye joto kali zaidi duniani.

Takwimu za Umoja wa Ulaya zinaonyesha kuwa gharama za uharibifu wa miundombinu na majengo barani Ulaya kutokana na hali mbaya ya hewa umekadiriwa kufikia dola bilioni 53.34 kwa mwaka, hii ikiwa ni mara tano zaidi kuliko miaka ya 1980.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW