1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Xi apigia upatu usuhuba wa China na mataifa ya Asia ya Kati

19 Mei 2023

Rais wa China Xi Jinping, amesema nchi yake pamoja na mataifa ya Asia ya Kati ni lazima yaanzishe kikamilifu ushirikiano wao katika sekta za biashara, uchumi, miundombinu na nishati.

Rais Xi Jinping akikutana na viongozi wa mataifa matano ya Asia ya Kati
Rais Xi Jinping akikutana na viongozi wa mataifa matano ya Asia ya Kati Picha: Florence Lo/REUTERS

Katika hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa viongozi wa mataifa hayo ya Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan, mjini Xian, kaskazini mwa China, Xi amesema kuna nia ya kuanzisha ushirikiano mwengine utakaoshajiisha ukuaji na maendeleo ya mataifa yote husika upande wa fedha, kilimo, kupunguza umasikini na utoaji wa hewa chafu, afya na masuala ya kidijitali.

Asia ya Kati imekuwa mshirika muhimu wa mradi mkubwa wa China wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri na barabara unaojulikana kama Belt and Road Initiative.

Xi anajaribu kuanzisha tena ushirikiano na mataifa hayo ili kuziba pengo lililopo katika mataifa hayo ya zamani ya muungano wa Kisovieti lililosababishwa na vita vya Urusi na Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW