1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Xi atoa wito kuzisaidia Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo

9 Julai 2024

Rais wa China Xi Jinping amemwambia waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban kuwa mataifa yenye nguvu duniani yanapaswa kuzisaidia Urusi na Ukraine kuanzisha tena mazungumzo ya moja kwa moja

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban (kushoto) asalimiana na Rais wa China Xi Jinping (kulia) kabla ya kufanya mkutano, Februari 13, 2014
Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban (kushoto) akutana na Rais wa China Xi Jinping (kulia)Picha: (Rolex dela Pena/Pool Photo/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la China CCTV limemnukuu Xi akisema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunda mazingira bora na kutoa usaidizi kwa Ukraine na Urusi ili kuanza tena kwa mazungumzo ya moja kwa moja.

Soma pia:Rais wa China Xi Jinping afanya ziara nchini Hungary

CCTV pia imeripoti kuwa Xi amemwambia Orban ni wakati tu ambapo mataifa yenye ushawishi yatakuwa na msukumo wa tija ndipo utakapokuwa mwanzo wa usitishaji haraka wa vita katika mzozo huo.

China ina ushawishi wa kuleta amani kati ya Urusi na Ukraine

Kufuatia mazungumza kati ya Orban na Xi, Orban aliandika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X kwamba China ni taifa lenye ushawishi katika kuunda mazingira ya amani kwenye vita vya Urusi na Ukraine.

Mkutano kati ya Orban na Xi waibua wasiwasi

Marekani imesema ina wasiwasi kuhusu mkutano huo kati ya Orban na Xi, huku msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby akisema ziara hiyo haionekani kuwa na tija katika suala la kujaribu kurekebsiha hali nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW