1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi atoa wito wa maelewano katika ujumbe wake kwa Trump

7 Novemba 2024

Rais Xi Jinping wa China amesema Beijing na Washington ni sharti zitafute njia ya "maelewano" katika ujumbe alioutuma kwa rais mteule wa Marekani, Donald Trump.

Donald Trump na Xi Jinping mwaka 2019
Donald Trump na Xi Jinping mwaka 2019Picha: Brendan Smialowski/AFP/Getty Images

Rais Xi Jinping wa China amesema Beijing na Washington ni sharti zitafute njia ya "maelewano" katika ujumbe alioutuma kwa rais mteule wa Marekani, Donald Trump.

Haya yameripotiwa na shirika la utangazaji la China, CCTV. Katika ujumbe wake wa kwanza kwa Trump tangu rais huyo wa zamani ashinde muhula wa pili jana, Xi amesema historia inaonyesha kwamba China na Marekani hunufaika kutokana na ushirikiano na kunakuwepo na hasara wanapozozana. Trump: Ninaweza kusitisha uhusiano na China kwasababu ya corona

Trump pamoja na Kamala Harris aliyekuwa mgombea wa chama cha Democratic, wote walikuwa wameahidi kuwa na misimamo mikali dhidi ya China.

Ila Trump aliongeza kwa kusema kuwa ataongeza ushuru kwa asilimia 60 kwa bidhaa zote za China zinazoingia Marekani.

China leo kupitia kwa msemaji wake wa wizara wa mambo ya kigeni, Mao Ning, imesema, "hakutokuwa na mshindi" katika vita vya kibiashara.