SiasaPeru
Xi, Biden kukutana kando mwa mkutano wa APEC nchini Peru
15 Novemba 2024Matangazo
Marais hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo hapo kesho kando ya mkutano huo wa siku mbili.
Kuna uwezekano kwamba hiyo ndio itakuwa mara ya mwisho kwa Biden kukutana na Xi akiwa kama rais, huku kukiwa pia na wingu la sintofahamu ya kidiplomasia kati ya Beijing na Washington kufuatia kuchaguliwa tena kwa Donald Trump.
Jumuiya ya APEC, iliyoundwa mwaka wa 1989 kwa lengo la kukuza biashara huria ya kikanda, inazijumuisha nchi 21 ambazo kwa pamoja uchumi wake unawakilisha takriban asilimia 60 ya pato la taifa la dunia na zaidi ya asilimia 40 ya biashara ya kimataifa.