1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Xi: China ´isichafuliwe jina´ kutokana na mzozo wa Ukraine

7 Mei 2024

Rais wa Xi Jinping wa China ameonya dhidi ya nchi yake ´kupakwa matope´ kutokana na mzozo wa Ukraine akisisitiza kwamba serikali mjini Beijing inatumia ushawishi wake kutafuta suluhu kwa njia ya amani wa vita hivyo.

Xi aliye ziarani nchini Ufaransa amewaambia waandishi habari akiwa na mwenyeji wake rais Emmanuel Macron, kwamba China inapinga kutumiwa mzozo wa Ukraine kama karata ya kuilaumu na kuchochea enzi mpya ya vita baridi.

Amesema China haijabikia kuwa mtizamaji na badala yake inafanya jitihada za kufanikisha kupatikana amani. Mbali ya mzozo wa Ukraine, rais Xi pia ametumia ziara yake ya Ufaransa kujadili masuala ya biashara na Ufaransa pamoja na kanda nzima ya Ulaya.

Hii leo Jumanne, Xi atasafiri na rais Macron kwenda jimbo la milimani la Pyrenees kabla ya kuelekea Hungary na Serbia kuendelea na ziara yake barani Ulaya.