Xi Jinping awasili Cambodia kwa ziara ya siku mbili
17 Aprili 2025
Xi atakutana na viongozi mbalimbali wa Cambodia ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Hun Manet aliyesema hivi majuzi kuwa China ni mshirika muhimu ambaye ameisaidia nchi hiyo kiuchumi na kijamii.
Biashara huenda ikawa katika ajenda ya mazungumzo
Biashara inaweza kuwa mada kuu ya majadiliano ya Xi huko Cambodia, ambayo inakabiliwa na viwango vya juu zaidi vya ushuru vilivyopendekezwa na Marekani.
Mbali na ushuru jumla wa 10% uliotangazwa na rais wa Marekani Donald Trump, nchi hiyo inakabiliwa na tishio la ushuruwa 49% kwa mauzo ya nje kwenda Marekani mara tu muda wa siku 90 wa kusitisha kutekelezwa kwa ushuru huo utakapokamilika.
Ziara ya Cambodia yahitimisha ziara ya Xi kusini-mashariki mwa Asia
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza tangu mwaka 2016, itahitimisha safari ya Xi kwenye nchi tatu za kusini-mashariki mwa Asia iliyozijumuisha Vietnam na Malaysia. Katika miaka ya hivi karibuni, Chinaimekuwa ikiongeza ushawishi wake katika eneo hilo kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kiuchumi.