1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi: Urafiki kati ya China, Hungary haulengi taifa la pembeni

9 Mei 2024

Rais Xi Jinping wa China amesema nchi yake iko tayari kwa pamoja kukuza kiwango cha juu maendeleo ya mahusiano na Hungary na urafiki wao si kulenga, wala kuamriwa na taifa au kundi lolote nje yao.

Ujumbe wa China na Hungary ukiwa katika meza ya mazungumza
Ujumbe wa China na Hungary ukiwa katika meza ya mazungumzaPicha: Noemi Bruzak/EPA

Rais Xi ameyasema hayo wakati wa ziara yake nchini Hungary taifa la mwisho la ziara yake kwa Ulaya baada ya Ufaransa na Serbia hapo mapema juma hili.

Soma pia:Rais wa China Xi Jinping afanya ziara nchini Hungary

Hungary chini ya waziri mkuu anayeegemea siasa za mrengo wa kulia Viktor Orban imekuwa mshirika muhimu wa biashara na uwekezaji wa China, tofauti na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya ambayo yanazingatia kutoitegemea sana nchi hiyo.
 


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW