SiasaAsia
Xi kuitembelea Korea Kaskazini wiki ijayo
5 Juni 2026
Matangazo
Vyombo vya habari vya China na Korea Kaskazini vimesema Xi atawasili mjini Pyongyang siku ya Jumatatu kwa ziara ya siku mbili.
Safari hiyo ni sehemu ya hatua kadhaa zinazochukuliwa na China kwenye kuimarisha mahusiano na taifa hilo jirani lenye silaha za nyuklia.
Inafanyika ikiwa zimepita wiki chache tangu Rais Xi alipowakaribisha Rais Donald Trump wa Marekani na baadaye Vladimir Putin wa Urusi mjini Beijing.
Tangazo kuhusu ziara ya Xi limetolewa siku moja baada ya Korea Kaskazini kuzindua kituo kipya cha kutengeneza vifaa vinavyotumika kuunda silaha za nyuklia, suala ambalo limekuwa chanzo cha mvutano wa muda mrefu kati ya nchi hiyo na Marekani.