1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi, Putin wasifu ushirikiano thabiti kati ya Urusi na China

4 Februari 2026

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, wamesifu ushirikiano thabiti wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili wakisema unatuliza hali katika nyakati hizi za mabadiliko na misukosuko

Urusi Moscow 2026 | Vladimir Putin katika mkutano wa njia ya video na Xi Jinping
Vladimir Putin katika mkutano wa njia ya video na Xi JinpingPicha: Kremlin Pool/Russian Look/picture alliance

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, wamesifu ushirikiano thabiti wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili wakisema unatuliza hali katika nyakati hizi za mabadiliko na misukosuko duniani.

Xi na Putin wameyasema hayo wakati walipozungumza hii leo kwa njia ya video. Mazungumzo hayo yamefanyika siku chache baada ya maafisa waandamizi kutoka nchi zote mbili kukubaliana kwamba uhusiano wao, unaweza kufungua ukurasa mpya mwaka huu wakati Moscow na Beijing zikiongeza ushirikiano wa kiuchumi.

Xi amemueleza Putin kwamba, tangu mwanzo wa mwaka huu, hali ya kimataifa imeendelea kuwa ya misukosuko zaidi, na kuongeza kuwa nchi zote mbili lazima ziimarishe ushirikiano wao katika mwelekeo sahihi.

Urusi na China zimejaribu kuonyesha mshikamano dhidi ya mataifa ya Magharibi, tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwaka 2022.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW