1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Xi: Apongeza ushirikiano mpya wa China na Colombia

25 Oktoba 2023

Rais wa China Xi Jinping amesifia ushirikiano mpya wa kimkakati kati ya nchi yake na Colombia.

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Colombia Gustavo Petro katika gwaride maalum.
Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Colombia Gustavo Petro katika gwaride maalum.Picha: Ken Ishii/Pool/AFP/Getty Images

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya China limeripoti hayo leo wakati Rais Xi alipomkaribisha mgeni wake rais wa Colombia Gustavo Petro.

Ikulu ya Rais Colombia ilisema Rais Gustavo aliyewasili China jana Jumanne, pamoja na mwenyeji wake Xi, watasaini mpango wa usitawi na uhusiano baina ya pande mbili.

Soma pia:Xi Jinping: Mradi wa BRI uko katika mwelekeo sahihi licha ya mivutano ya kimataifa

Rais Xi alimwambia Petro kwamba anafurahi kutangaza kwa pamoja uimarishaji wa ushirikiano wa China na Colombia kufikia ule wa kimkakati.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW